Log inLog Out
For YouNewsEntertainmentRelationshipLifestyleSportTechnology
Serikali kuimarisha usafiri wa majini.

Fatman

July. 07, 2020

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema malengo ya Serikali ni kuimarisha usafiri kwenye maziwa yote na bahari ili kuwawezesha Watanzania wafanye biashara na mataifa ya nje.
Akizungumza na wananchi katika viwanja vya Klabu ya Bandari mjini Mtwara Waziri Mkuu amesema  kabla ya kukagua ujenzi wa gati namba 2 katika bandari ya Mtwara juzi alitembelea miradi ya ujenzi wa bandari za Karema (Katavi), Kabwe na Kasanga (Rukwa) katika mwambao wa Ziwa Tanganyika.
Amesema katika Ziwa Victoria kuna meli iliyokuwa inakarabatiwa na imeanza majaribio ya kwenda Kagera na nyingine inaendelea kujengwa ili kuruhusu wafanyabiashara wa Kanda ya Ziwa wafanye biashara zao kwa urahisi.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amewataka vijana wanaopata ajira kwenye miradi mikubwa inayogharimiwa na Serikali watumie fursa hiyo kupata utaalamu utakaowawezesha kuajiriwa maeneo mengine hata baada ya miradi ya sasa kukamilika.
0
Comments
Sign in to post a message
You're the first to comment.
Say something
Recommend
Log in