Back
Tshishimbi: Nitarudi nyumbani DR Congo
Aug 1, 2020
Nahodha na kiungo wa klabu ya Young Africans Papy Kabamba Tshishimbi amesema yupo tayari kurejea nyumbani kwao DR Congo, kama klabu hiyo haitokua tayari kuendelea naye kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Tshishimbi ameyasema hayo kufuatia sakata linaloendelea katika vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii, ikidaiwa kiungo huyo amekataa kusaini mkataba mpya, kwa madai ya kuhitaji kiasi kikubwa cha pesa, tofauti na aliyoahidiwa na uongozi.
Kiungo huyo amesema Kaimu Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Wakili Patrick Simon, licha ya kuwa mwanasheria hajui mambo ya soka kutokana na kwenda kuuzungumzia mkataba wake kupitia redio moja jijini Dar es Salaam.
Awali katika sakata hilo, kiungo huyo alisema bado hajasaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia timu hiyo, na alipoulizwa Simon, alikiri ni kweli na kwamba wamempa siku 14 Mkongomani huyo kufanya uamuzi kuhusu hatima yake ya kusaini ama la.
Simon alisema: “Alifanya mazungumzo na makubaliano yalifikiwa, bado tu kusaini mkataba mpya, baada ya mazungumzo hayo,
Hersi Said (GSM) alitueleza viongozi, lakini uongozi wa klabu nao ulitoa mapendekezo yake juu ya kiasi anachokitaka Tshishimbi na tulisema tukipunguze na tumempa siku 14 ambazo zitamalizika Jumatano wiki ijayo,” alisema kiongozi huyo.
Lakini baada ya taarifa hiyo, Tshishimbi ameibuka na kumponda kiongozi huyo kwa hatua ya kuuzungumzia mkataba wake redioni huku akishangaa kuambiwa amepewa siku 14 kitu ambacho hajaelezwa.
5Shares
0Comments
0Favorites
0Likes
Say something to impress...
Loading...
Comments
Hot

No content at this moment.

Relevant people
Mseto
18580 Followers
Taarifa kwa utendeti
Related