Back
Orodha ya Vilabu Bora Afrika 2025 (CAF Club Ranking)kwa sasa.
Apr 14, 2025
Katika viwango vya vilabu bora barani Afrika kwa mwaka 2025, Simba SCkutoka Tanzania imepanda hadi nafasi ya nne baada ya kufanya vizuri katika michuano ya CAF Confederation Cup na CAF Champions League. Hii ni hatua kubwa kwa klabu hiyo, ambayo imeendelea kuonyesha ubora wake katika mashindano ya kimataifa.
Vilabu 10 Bora Afrika 2025
Kwa mujibu wa viwango vya CAF, vilabu bora barani Afrika kwa mwaka 2025 ni:
Al Ahly SC (Misri) – 78 Points
Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) – 57 Points
Esperance de Tunis (Tunisia) – 57 Points
Simba SC (Tanzania) – 43 Points
RS Berkane (Morocco) – 42 Points
Zamalek SC (Misri) – 42 Points
Wydad AC (Morocco) – 39 Points
Pyramids FC (Misri) – 37 Points
USM Alger (Algeria) – 37 Points
CR Belouizdad (Algeria) – 36 Points
Simba SC imepanda kutoka nafasi ya sita hadi nne, ikiwa nyuma ya Al Ahly, Mamelodi Sundowns, na Esperance de Tunis. Hii ni kutokana na mafanikio yake katika hatua ya robo fainali ya michuano ya CAF, ambapo ilifikisha pointi 43 kwenye ubora wa vilabu Afrika.
Mabadiliko Katika Viwango
Katika orodha ya mwaka huu, Simba SC imepanda hadi nafasi ya 4 baada ya kufanya vizuri katika CAF Champions League, ikimshusha RS Berkane kutoka nafasi ya 5. Aidha, Young Africans SC (Yanga SC) imepanda hadi nafasi ya 11 kutoka nafasi ya 13, baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika mashindano ya kimataifa.
2Shares
0Comments
2Favorites
17Likes
No content at this moment.