Back
Fei Toto Akataa Mshahara Wa Milioni 80
May 15, 2025
Msimu wa Ligi Kuu Bara ni kama umebakiza mechi zisizozidi tano kwa timu zote kuhitimish-wa, lakini kuna harakati kibao zinazoendelea kwa kila timu kuweka hesabu zake sawa katika dakika hizi za lalasalama.
Wakati ukisoma hapa, nyuma ya pazia la timu hizo kuna vita ya kuwania kiatu cha mfungaji bora wa ligi, mchezaji bora, kipa bora na hata timu pia kuvizia tuzo mbalimbali ifikapo mwisho wa msimu.
Lakini, kwa sasa ukienda katika ofisi za klabu ya Azam, kuna mkataba mnono upo mezani wenye thamani ya Sh3.1 bilioni ukimsubiri kiungo fundi wa kikosi hicho, Feisal Salum ‘Fei Toto’ kum-waga wino kuendelea kuitumikia timu hiyo kwa miaka miwili zaidi.
Hata hivyo, mkataba huo ambao upo mezani tangu Machi mwaka huu baada ya majadiliano ya mwisho, bado Fei Toto ameukaushia huku ikionekana hayupo tayari kuendelea kuitumikia Azam.
Wakati Fei Toto akiukaushia mkataba huo, uongozi wa Azam nao umeonekana kurusha taulo juu ya kuendelea kumshawishi kiungo huyo kusalia katika viunga vya Chamazi huku kukiwa na taa-rifa za Simba, Yanga na Kaizer Chiefs zinaiwania saini yake.
Fei ambaye mkataba wake na Azam umebaki msimu mmoja ukitarajiwa kumalizika 2026, ali-jiunga na timu hiyo Julai 2023 akisaini mkataba wa miaka mitatu akitokea Yanga.
Taarifa kutoka ndani ya Azam zinabainisha kuwa katika mkataba ambao uongozi wa klabu hiyo umemuwekea Fei, kuna kipengele cha mshahara mnono wa Sh80 milioni kwa mwezi, ada ya usajili na kuwa balozi wa bidhaa za kampuni za Azam.
13Shares
0Comments
5Favorites
22Likes
No content at this moment.