Log inLog Out
EntertainmentRelationshipLifestyleSportTechnology
Walimu wakuu watakiwa kusimamia vitendo maelekezo yaliyotolewa na wizara ya elimu pamoja na wizara ya afya

Khadija Mussa

July. 03, 2020

Mkuu wa wilaya ya kaskazin B Rajab Ali Rajab amewataka walimu wakuu wa skuli za wilaya hiyo kusimamia kwa vitendo maelekezo yaliyotolewa na wizara ya elimu pamoja na wizara ya afya kwa kuhakikisha kila darasa lina wanafunzi wasiozidi 40.
DC amesema hayo  katika ziara aliyoifanya hivi karibuni katika skuli mbalimbali za wilaya hiyo na amegundua kuwepo kwa tatizo la usimamiaji  kwa wanafunzi  kwani wamekuwa wakikaa bila ya kufuata utaratibu uliowekwa na serikali.
Akizungumza katika kikao cha walimu wakuu ,walimu wa madrasa pamoja na maimamu huko mahonda Rajab amesema licha ya serikali kurudisha huduma zote ikiwemo suala la elimu lakini bado ipo haja kwa walimu hao kuwa makini katika kipindi chote cha ufundishaji.
Akizungumzia  suala la elimu ya madarsa amesema hadi sasa bado elimu hiyo haijaruhusiwa hivyo ni vyema kwa walimu hao kuendelea kustahamili mpaka pale ofisi ya mufti itakaporudisha tena huduma hiyo Amefahamisha kuwa serikali inatambua umuhimu wa elimu hiyo lakini inahitaji kuweka utaratibu mzuri  utakaoondoa msongamano katika madrasa hizo.
Hata hivyo amewataka maimamu wa miskiti kuisaidia serikali kutoa elimu kwa mahujaji waliotarajia kufanya hija mwaka huu kuwa ibada hiyo imesitishwa mpaka pale gonjwa la corona litakapomalizika Kwa upande wa vitendo vya udhalilishaji mkuu huyo wa wilaya kuendelea kushirikiana pamoja ili kudhibiti vitendo hivyo visiendelee kuathir jamii ya wanawake na watoto ambao ndio waathirika wakubwa wa Vitendo hivyo.
Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa kikao hicho wamesema bado kuna uelewa mdogo kwa wazazi kuhusu uvaaji wa barkoa kwa watoto wao pamoja na kuwepo tatizo la ukosefu wa maji katika baadhi ya skuli hali ambayo inasababisha kushindwa kutekeleza kwa vitendo maagizo ya serikali.
Rauhiya Mussa
0
Comments
Sign in to post a message
You're the first to comment.
Say something
Recommend
Log in