Log inLog Out
For YouNewsEntertainmentRelationshipLifestyleBusiness
Mabinti 2 Wamuua Baba Yao Kwa Sababu Ya Ksh 5,000

Bertillar

Dec. 01, 2019

Dada wawili kutoka kaunti ya Embu walifikishwa mahakamani Ijumaa, Novemba 29 baada ya kushukiwa kwa kumuua baba yao Esther Kagendo Mwangi, 28, na Emily Wanjira Mwangi, 24, waliripotiwa kumshambulia baba yao kwa kumpiga na kifaa butu hadi akafariki.
Dada hao walimkashifu baba yao kwa kutumia pesa walizokuwa wamechanga ili kugharamia mazishi ya kaka yao mwenye umri wa miaka 19 aliyeaga dunia baada ya kuugua kwa muda mchache.
Mama yao Tabitha Weruma pia alikashifiwa kwa kushirikiana na mabinti wake kumuua mumewe.
Kulingana na Tabitha, mumewe Zachary Kiura Mutindi alitumia pesa hizo kununua pombe baada ya kutoweka nyumbani kwa siku 3.
Mutinda na mwanawe walizikwa siku moja nyumbani kwa kaunti ya Embu.
0
Comments
Sign in to post a message
You're the first to comment.
Say something
Recommend
Log in