Log inLog Out
For YouNewsEntertainmentRelationshipLifestyleBusiness
Hakuna Kutembea Uchi!! 'Shosh' Awavua Akina Dada Waliovalia Minisketi Jijini Nairobi

Bertillar

Dec. 05, 2019

Mwanamke mmoja wa umri wa makamo amewaacha wakazi wa Nairobi kwa mshangao baada ya kunaswa kwenye video akizunguka jijini akiwavuta wanadada waliokuwa wamevalia minisketi.
Bibi huyo alisema mavazi yoyote juu ya magoti ni ya kishetani na yuko katika operesheni ya kusanifisha maovu dhidi ya fasheni hiyo.
Katika video hiyo iliyosambaa kwenye mtandao jamii, mwanamke huyo anasikika akipiga kamsa huku akijaribu kuburuta sketi ya mwanadada mmoja katika eneo la Moi Avenue. Mama huyo alikuwa amevalia sketi ndefu huku mwathiriwa aliyejaribu kumuaibisha akiwa amevalia minisketi nyeusi.
Wakenya waliotazama video hiyo walidai mama huyo ni mhubiri ambaye hupatikana kila mara katika barabara ya Mama Ngina Street. Mhubiri huyo huambatanisha mahubiri yake na matusi yanayowalenga akina dada kwa kuvalia minisketi na longi za jeans.
Mama huyo anadaiwa kuendesha mahubiri katika barabara ya Mama Ngina na kuwatusi wanawake ambao huvalia minisketi.
0
Comments
Sign in to post a message
You're the first to comment.
Say something
Recommend
Log in