Log inLog Out
For YouNewsEntertainmentRelationshipLifestyleBusinessTechnology
Huduma Za Bodaboda Zapigwa Marufuku Kwa Wiki Mbili Huko Machakos

Mary KE

March. 23, 2020

Gavana wa Machakos, Alfred Mutua amepiga marifuku huduma zote za boda boda pamoja na tuk tuk katika kaunti hiyo kama njia ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona. Katika taarifa siku ya Jumatatu, Machi 23, Mutua alisema huduma hizo zimesimamishwa kwa wiki mbili kuanzia Jumatano, Machi 25, na pia kuongezea kuwa hawatalipa ushuru miezi iliyosalia mwaka huu.
“Kuanzia Jumatano, Machi 25, saa kumi na moja asubuhi, hakuna Boda Boda, Maruti ama Tuktuks zitaruhusiwa kuhudumu Kaunti ya Machakos kwa wiki mbili. Hatuwezi kutimiza sheria ya kukaa mbali kama tunatumia Boda Boda kwani abiria hukaribiana na dereva,” “Ili kuwalipa fidhia kwa hali hiyo ama kupoteza mapato, serikali yangu itaondoa ushuru yote ya Boda Boda, Maruti na Tuk Tuk kwa siku siku zilizosalia hadi Disemba 31 2020," alisema.
Mutua pia amepiga marufuku siku za soko, vikao vya miraa na muguka na pia makundi ya watu zaidi ya watu watatu katika kaunt hiyo. Wakati huo huo, wakazi wa Machakos wameagizwa kusalia manyumbani kwao na pia kuwa nyumbani kufikia saa moja usiku huku wale wa miaka 65 wakishauriwa kujiepusha na kutangamana na watu wachanga na watoto hususan wa kutoka mijini.
-Tuko
0
Comments
Sign in to post a message
You're the first to comment.
Say something
Recommend
Log in