Log inLog Out
For YouNewsEntertainmentRelationshipLifestyleBusiness
‘Mama yangu marehemu ndiye anajua baba yangu,’ Jamaa anaye fanana na Uhuru hatimaye azungumza

i can t sleep

Aug. 09, 2020

Baada ya picha zake kusamba na kuenea sana kwenye mitandao ya kijamii wanamitandao  waliibua hisia mseto kuhusu picha hiyo ya mwanamme ambaye anafanana na rais Uhuru Kenyatta.
Hatimaye jamaa huyo amezungumza kwa mara ya kwanza tangu picha hizo kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Hakika wengi walidhani kuwa picha za Michael Njogo Gitonga, ni za Uhuru mwaka wa 2013 kabla hajawa rais wa Kenya.
Akiwa kwenye mahojiano Njogo alisema sasa inambidi kuficha uso kutumia maski kwani ingawa kuna virusi vya corona vinavyofaa kudhibitiwa, maski inamsaidia kujificha ili asije kuangaliwa kila mara na watu wanaomfananaisha na Rais Uhuru Kenyatta.
Kutokana na sura inayofanana zaidi na ya rais, watu mtaani kwake Umoja, Nairobi wamempachika jina “Uhunye”.
Ingawa hana nguvu alizonazo rais wa Jamhuri ya Kenya, Njogo anafurahia umaarufu aliopata ambao umejiri na uzito fulani.
“Siwezi kutembea mitaani kawaida bila ya watu kuniomba niwape kitu kidogo, napata taabu na jina hili Inanishangaza kiukweli, kwani najiuliza maswai ni kwa nini nafanana na Rais Kenyatta, si kitu cha kawaida.” Alizungumza Njogo.
Wakati picha zake zilipokuwa sikisambaa mtandaoni, kuna baadhi ya watu waiodai labda picha hizo zilikuwa zimefanyika ‘photoshop’ huku wengine wakimtaka afanye Uchunguzi wa Asili nasaba (DNA) kuthibitisha ukweli wa mambo.
Njogo alisema kuwa akipata fursa ya kukutana na Uhuru Kenyatta atamuuliza iwapo wao ni kaka.
Akiwa mwashi, kazi yake ya ufundi anasema hajakuwa akiifanya na kwamba baa yake mtaani Umoja biashara imedorora mno tangu zilipofungwa kutokana na janga la Covid-19.
Njogo alisema, anaamini na kutarajia siku moja ukweli utabainika kuhusu nani baba yake mzazi kwa kuwa mtu wa pekee anayefahamu kwa wazazi wake ni mama ambaye ni marehemu.
0
Comments
Sign in to post a message
You're the first to comment.
Say something
Recommend
Log in