Back
WANAFUNZI SAVANNAH PLAINS WAELEKEA NAIROBI KENYA KUSHIRIKI MASHINDANO YA UBINGWA WA DUNIA YA KUONGEA KWENYE HADHARA
May 8, 2024
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Savannah Plains iliyopo Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga Mkoa wa Shinyanga nchini Tanzania wamesafiri kuelekea Jijini Nairobi nchini Kenya kushiriki Mashindano ya Ubingwa wa Dunia wa Mjadala na Kuongea kwenye hadhara kwa kutumia lugha ya Kiingereza (World Championship Debate and Public Speaking Tournaments) yatakayofanyika kuanzia Mei 9,2024 hadi Mei 13,2024.
Uongozi wa shule umeweka wazi kuwa msafara una jumla ya wanafunzi 25, ambapo Mratibu wa somo la Kiingereza ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Lugha katika Shule ya Sekondari Savannah Plains , Josephine Kinyunyi anasema kutokana na maandalizi waliyoyafanya wanatarajia kupata ushindi katika mashindano hayo ya kidunia na kuendelea kuipa heshima na kuitangaza nchi ya Tanzania kimataifa.
"Tunaelekea nchini Kenya kwa ajili ya kushiriki Mashindano ya Ubingwa wa Dunia wa Mjadala na Kuongea kwenye hadhara kwa kutumia lugha ya Kiingereza (World Championship Debate and Public Speaking Tournaments) ambayo ni mwendelezo wa mashindano ya Mjadala na Kuongea kwenye Hadhara kwa kutumia lugha ya Kiingereza (Johannesburg Summer Holiday Open Debate and Public Speaking Tournaments ) yaliyofanyika katika Jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini kuanzia Desemba 11 hadi 19, 2023 ambayo Savannah Plains tulishinda tukapata nafasi ya kushiriki mashindano haya ya Dunia, kwa hiyo tunaenda Kenya kwa ajili ya hayo mashindano",amesema Josephine.
12Shares
0Comments
2Favorites
9Likes
No content at this moment.