Back
Wananchi wapatao 8,512, 952 waishio vijini watanufaika na huduma ya mawasilino pindi ujenzi wa minara 758 nchini utakapokamilika mwaka 2025 na kuwawezesha kupata huduma mbalimbali za mtandao. Hayo yamesemwa leo Julai 15, 2024 katika kikao cha kupokea taarifa za mawasiliano kwa mkoa wa Kigoma baada ya Waziri wa Habari na Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye kuanza ziara ya siku moja mkoani humo. Nape ameanza ziara ya kukaguwa kazi za ujenzi wa minara hiyo kwa mikoa ya Kigoma, Kagera, Geita, Mwanza na Shinyanga. Amesema kukamilika kwa minara hiyo kutatoa fursa kubwa kwa wananchi wa vijijini kwani nao wana haki ya msingi ya kupata mawasiliano kama wananchi wa maeneo mengine katika uchumi wa kidigitali. #CloudsDigitalUpdates
Jul 15, 2024
12Shares
0Comments
7Favorites
17Likes
No content at this moment.