Back
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amesema “ilikuwa awe amekufa” baada ya jaribio la kumuua kushindikana mnamo siku ya Jumamosi katika mkutano wa hadhara huko Pennsylvania.-Katika mojawapo ya mahojiano yake ya kwanza tangu kisa hicho kimtokee, Bw Trump aliviambia vyombo vya habari kuwa alihisi ameokolewa “kwa bahati na Mungu”. -Trump anasema “Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba sikugeuza tu kichwa changu lakini kugeuka kwa wakati ufaao na kwa kiwango kinachofaa,” alisema, kuwa risasi ilivyogusa sikio lake ingeweza kumuua kwa urahisi. “Ninapaswa kufa, sitakiwi kuwa hapa huu ni mpango wa mungu tu” alisema Trump.-Mtazamaji mmoja aliuawa katika shambulio hilo, huku watu wengine wawili wakijeruhiwa vibaya. Mshambuliaji, ambaye pia alikufa, alifahamika kwa jina la Thomas Matthew Crooks.-#EDigital #RunForPresident #Trump #TveTanzania
Jul 15, 2024
5Shares
0Comments
10Favorites
17Likes
No content at this moment.