Back
cloudstv
Clouds TV
25/7 Watanzania kote nchini wanaungana kwa pamoja kuadhimisha Siku ya Mashujaa, siku maalum inayotolewa kwa heshima ya wale wote waliotoa maisha yao, muda wao, na ujasiri wao kwa ajili ya kulinda uhuru, amani na hadhi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Katika maadhimisho ya mwaka huu, heshima ya kipekee imemwagiwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambalo linaendelea kutajwa kuwa nguzo kuu ya ulinzi wa taifa na mfano wa mashujaa wa kweli wa karne hii.Katika upepo wa asubuhi wa tarehe 25 Julai 2025, ardhi ya Tanzania inazizima kwa heshima, Midomo ya Watanzania inazungumza kauli moja “Shujaa haachi alama tu ardhini, huacha hadithi mioyoni." Na hadithi kubwa zaidi tunayoiadhimisha leo ni ile ya mashujaa wetu Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).Hawa si watu waliovaa sare tu La hasha! Hawa ni walinzi wa matumaini, wasimamizi wa Amani, wapiganaji wa haki, na mabingwa wa mshikamano. Wakivalia sare zao za kijeshi, si tu wanajiandaa kwa vita, bali huvaa dhamira ya kulinda kila tone la uhuru tuliourithi kwa jasho na damu.Tofauti na majeshi mengine Jeshi la Wananchi wa Tanzania halivumi, lakini hutetemesha, Ni jeshi linaloheshimu sheria, siyo linaloburuza, ni jeshi la wananchi, lililozaliwa kutoka kwenye matakwa ya uhuru na lisilojitenga na wananchi.Ndilo linalochunga mpaka wa Kagera hadi Mtwara, kutoka Tunduma hadi Mikanjuni ya Tanga kwa macho yasiyolala.Wanajeshi wetu hawasubiri vita kuvuma, Wanaishinda hata kabla haijaanza kwa mafunzo, uadilifu, na utayari usiotikisika. Kila doria ni ahadi, kila zoezi ni kiapo, na kila operesheni ni ibada ya taifa.Mashujaa hawa wamepitisha kivuli cha bendera ya Tanzania mbali na mipaka yetu. Ni nani huyu atakayesimama mbele ya shujaa wa JWTZ na kusema “sijasikia huduma yako?”Heri ya Siku Mashujaa Mtanzania, jivunie kulindwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ, Mashujaa wa Taifa walinzi wa Dunia.✍🏻 @azizi_kindamba
Jul 25, 2025
12Shares
0Comments
5Favorites
19Likes
Say something to impress...
Loading...
Comments
Hot

No content at this moment.

Relevant people
cloudstv
982 Followers
others
Clouds TV
Related