Log inLog Out
Local NewsEntertainmentRelationshipLifestyleTechnology
TCB yaagizwa kujenga ghala la kuhifadhia na kuuza kahawa.

Adeleye Simon oye

July. 03, 2020

MOSHI KILIMANJARO.
Naibu Waziri wa Kilimo , Mhe.Hussein Bashe ameiagiza Bodi ya Kahawa Tanzania kwa ushirikiano na Benki ya Kilimo Tanzania kujenga ghala la kuhifadhia na kuuza kahawa iliyosindikwa nchini China.
Ametoa agizo hilo alipotembea Bodi ya Kahawa kuona shughuli za uendeshaji wa mnada unavyokuwa katika Soko la Dunia na kuzungumza na wafanyakazi na menejmenti ya bodi hiyo.
Mhe.Bashe amesema kwa kujenga ghala hilo na kuuza kahawa iliyosindikwa katika nchi hizo kutasaidia kupanua wigo wa soko la Kahawa ya Tanzania ambayo inapendwa na mataifa mengi duniani.
Hata hivyo Naibu Waziri wa kilimo ambaye alikuwepo kwa ziara ya siku mbili kuzitembelea taasisi zilizo chini ya wizara yake ameahidi kurejea tena kutokana na muda mfupi aliokuwa nao.
0
Comments
Sign in to post a message
You're the first to comment.
Say something
Recommend
Log in