Back
NBC yatambulisha mikopo kwa wajasiriamali isiyo ya dhamana
Jul 9, 2020
Kadhalika, lengo ni  kuunga mkono jitihada za serikali katika kufanikisha uchumi wa viwanda.
Akizungumza kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa benki hiyo,  Elvis Ndunguru, alisema mikopo hiyo  inawalenga wajasiriamali wenye zabuni za kampuni kubwa.
“NBC tumechukua hatua hii ili kuwasaidia wajasiriamali wadogo na wa kati kwa kutambua kwamba kwa kuwawezesha ndio tutakuwa tunaisaidia pia serikali kufanikisha agenda yake ya uchumi wa viwanda,” alisema.
Hatua ya benki hiyo inakuja huku tafiti zikionyesha wajasiriamali wadogo na wa kati wanashikilia asilimia 95 ya biashara zote nchini na ni moja ya sekta zinazokua kwa kasi zaidi kiuchumi, huku ikichangia asilimia 35 ya Pato la Taifa (GDP).
"Hivyo basi, NBC tumeona kuna umuhimu wa kukua sambamba na sekta hii ambapo tumekuwa tukifanya tafiti mbalimbali za kimasoko ili  kutoa huduma sahihi za kifedha zinazozingatia mahitaji yao kuelekea mafanikio ya ukuaji wa kiuchumi,” alisema.
Alisema benki hiyo ilitoa mafunzo sambamba na kutoa mikopo yenye thamani zaidi ya Sh. bilioni 80 kwa wajasiriamali takribani  3,000 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita pekee, huku akibainisha kuwa benki hiyo inatarajia kutoa mikopo zaidi.
Alizitaja sekta ambazo zimenufaika na mikopo hiyo  ni za biashara, makandarasi, mafuta na gesi, utalii na hoteli, usafirishaji, viwanda na kilimo.
2Shares
0Comments
0Favorites
2Likes
Say something to impress...
Loading...
Comments
Hot

No content at this moment.

Relevant people
Dira Ya Scooper
7792 Followers
Darubini ya Ulimwengu
Related